Mambo mazuri yanayofanywa na mafuta ya nazi kwako mrembo



Mafuta ya nazi ni moja ya bidhaa za asili zenye matumizi yanayoleta matokeo mazuri katika urembo na afya kwa ujumla.Ukizingatia kwamba ni mafuta yanayopatikana kirahisi na pia hata yakichujiwa viwandani na kufungashwa bado bei yake ni nafuu sana ukilinganisha na faida zake katika ulimwengu wa urembo.

Yafuatayo ni baadhi tu ya matumizi ya mafuta ya nazi

  • Ni mafuta ya kipekee ya msingi ya ngozi, yaani ukiwa nayo basi ngozi yako iko vizuri huhitaji kuyaongeza kitu chochote. 
 

  •   Husaidia kuondoa harufu mbaya mwilini yanapopakwa, inasemekana yana uwezo wa kuua bakteria wanasababisha harufu mbaya. Paka kama dozi kila siku, harufu inaondoka na ngozi ya sehem husika inalainika. Wale wa kikwapa na harufu za sehemu za siri hupona ukitumia mafuta ya nazi kupaka sehemu husika. Pia kwa sehemu nyingine unaweza kutumia kwa kuchanganya na baking soda ili kuondoa harufu mbaya.

 Mafuta ya nazi yanasaidia kuondoa make up iliyogandia mfano make up za machoni na lipstick kavu.





  • .Mafuta ya nazi yanasaidia kumkinga mtu dhidi ya stretch marks wakati wa ujauzito inafanya vizuri ukiichanganya na cocoa butter. 

  • Mafuta ya nazi yanaweza kutibu maambukizi ya fungus(yeast, candida) kwa kupaka kwenye sehemu iliyoathirika. Unaweza kuyatumia kwa ajili ya massage ya mwili
  • Ukipaka mikononi na miguuni yanasaidia kuondoa ukavu. Miguuni unaweza kutengenezea scrub kwa kuchanganya na chumvi.
  •  Yanafaa katika kupendezesha nywele zako( yanang'arisha na kuzifanya nywele kuonekana zina afya) usipake mengi kwenye nywele: paka kwenye ngozi ya kichwani kwa ajili ya kuzipa nywele zako afya na kasi ya kukua.
 
 
  • Unaweza kupaka mafuta ya nazi usiku kwa ajili ya kulainisha ngozi yako.
  • Mafuta ya nazi ukichanganya na sukari kutengeneza uji mzito inatumika kama scrub ya kulainisha ngozi yako.
  • Ukipaka midomoni yanasaidia kuondoa kukauka kwa midomo.
  • Mafuta ya nazi yanasaidia kupona kwa vidonda na kupotea kwa makovu haraka.
  • Unaweza kuyatumia mafuta ya nazi kama hair conditioner kwa ajili ya nywele kavu: Paka mafuta ya nazi kwenye nywele zako kavu kisha vaa kofia ya plastic au rambo na kaa nayo kichwani kwa masaa kadhaa hata mawili ndo utoe. nywele zako zinalainika na kuchanika kirahisi.
  •  
  • Mafuta ya nazi yanaweza kusaidia kuikinga ngozi yako na ukavu wa kuungua na jua kali.

  • Mafuta ya nazi yanaweza kupakwa baada ya kunyoa kama after shave lotion kwa ajili ya kuipa ngozi yako hali nzuru na kuzuia vijipele.
  • Yanaweza kuasaidia kutibu chunusi yakitumiwa kwa ratiba maalumu, kiasi kidogo tu. Fatty acids Lauric acid na capric acid katika mafuta ya nazi inasemekana zinasaidia kutibu chanzo cha chunusi. Yasugue mafuta yako kwenye viganja kisha paka usoni, utang'aa lakini yanafyonzwa haraka yanapotea mda mfupi hayana tabia ya kunona. Hakikisha ngozi yako ni safi kabisa kabla ya kupaka.
  •  
  •  Mafuta ya nazi yanaweza kutumika kupunguza muonekano wa kuzeeka kwa ngozi.
  • Mafuta ya nazi yanaweza kusaidia kucha zikue ukipaka eneo linalozunguka kucha zako.
  •  Ukipakaa kwenye maungio yanasaidia kulainisha ngozi za sehemu hizo.
  •  Mafuta ya nazi yakichanganywa na shea butter yanakuwa na nguvu zaidi katika kulainisha ngozi ya mwili mzima.
  • Ukitoka kufua au kuosha vyombo paka mafuta ya nazi kwa ajili ya kuilainisha ngozi yako.
Vitu vya asili kama hivi huzipa ngozi zetu afya na kupendeza bila madhara yoyote.

Nakutakia mafanikio katika kutumia vizuri mafuta ya nazi. 

No comments:

Post a Comment

Adbox

@EmmyGraphicsPrinting