Kuwajenga wasichana

 Nr.10 1 LEARNING BY EAR EPISODE – Girls 10th Episode: Beauty Text: Zainab Aziz Redaktion: Andrea Schmidt/Christine Harjes CHARACTERS: Anchor: Intro / Autro Bibiy..........Main Character. Alma.......Same Character. Rossie.......Same Character. Beautician.....woman adult Head Teacher........Same Character in episode..1 Timo.......Same Character Kibegu.....same Character. Into: Karibu tena msikilizaji kwenye mfululizo wa makala ya Jifunze Kwa Kusikiliza..mchezo huu wa hadithi unaangazia maswala mbali mbali yanayowakabili wasichana. Karibu kwenye sehemu ya kumi ya mchezo huu ambapo leo hii Bibiy na wenzake wanauangalia urembo kwa kwa wasichana. Sign Tune...... SCENE ONE: BIBIY: Loo! Alma ...Unafanya nini rafiki yangu? Hebu angalia sura yako.. (anacheka) ...Umejipaka nini? ALMA: Aaah!! Bibiy hebu wacha kunicheka, mwenzio najaribu kujipamba kwani umesahau kuwa sherehe ya mwaka ya shule yetu imekaribia.. ndio maana najaribu kujipodoa ili siku hiyo nitoke kweli kweli. BIBIY: Ndio!! Alma sikatai.. lakini ni nani aliyekwambia kuwa urembo ni mpaka ujipake madude namna hiyo Eeeh!!! ..(anacheka tena) Yaani mimi siwezi kunyamaza kwa Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 2 sababu unanichekesha...loo unanivunja mbavu. unakaa kama kinyago. ALMA: Basi bwana Bibiy ...usinicheke namna hiyo, mwenzio nataka kuwa kama wale mabinti urembo..unajua natamani sana kuwa model ... ni ndoto yangu kuwa siku moja niwe model maarufu. BIBIY: Hiyo ni ndoto nzuri Alma lakini huna haja ya kujisumbua namna hii..hata hiyo siku ya sherehe ya mwaka ya shule ukitokea namna hiyo rafiki yangu.. nakwambia mbona kila mtu atakukimbia. ALMA: Ok!! ... Bibiy haya basi umeshinda na mimi nakubali nimeshindwa na hivi nakwenda kuosha uso wangu..(Maji yanasikika yakitiririka kutoka kwenye mfereji)..haya nimeshaosha uso wangu niambie sasa kipi kinachofuata? BIBIY: sawa, sasa tunakwenda kumtembelea mke wa Yule msimamizi wa internet cafe..yeye ni mtaalamu wa urembo na Salon yake iko pale pale karibu na internet cafe tunayokwenda kila siku..huko Alma tutajifunza mengi kuhusu urembo na pia tunaweza kuuliza maswali jinsi tunavyopenda..pia huyo Aunty amekubali kutusaidia kuandaa maonyesho mitindo ya mavazi na urembo katika sherehe yetu ya mwaka shuleni. ALMA: hapo sasa unaniambia habari nzuri kweli, ndio maana nakupenda rafiki yangu Bibiy..wewe kila wakati huwa hukosi suluhisho kwa tatizo lolote lile..bila wewe rafiki yangu sijui ningekuwa wapi mimi..eenhe. sasa tunapitia kwa akina Rossie ili tumchukue twende naepamoja au vipi? BIBIY: Hata hatuna haja ya kumpitia kwao mbona anatungojea kwenye kituo cha basi..wewe harakisha kwani tumechelewa. MUSIC (Barabarani.. magari, honi na watu wanazungumza) Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 3 ALMA: Hee mwangalie Rossie yule!! Natumai hakutungoja kwa muda mrefu, maanake atapiga kelele huyo mpaka kila mtu atasikia kuwa tumechelewa. BIBIY: Hatutampa nafasi ya kuanza kulalamika sisi ndio tutaanza kumuomba msamaha..nyanya yangu aliniambia kuwa, ukijua umemkosea mwenzio basi haraka muombe samahani kwa kuwa ukifanya hivyo utaepusha mgogoro..na mwenzio atakuwa hana sababu ya kukasirika, kwa hivyo sisi tumuombe msamaha Rossie. ROSSIE: Hee !! wasichana nyie mbona mmechelewa namna hii mimi niliku...? (Bibiy anamkatiza) BIBIY: Usijali sana Rossie hebu tulia kidogo!! ... tunaomba samahani kwa kukuweka hapa kwa muda mrefu pole sana rafiki yetu..na sasa tunaweza kuendelea na safari yetu. ROSSIE: Ok!! Vizuri umenituliza hasira yangu kwa sababu nilikuwa nachemka..enhee niambieni basi kitu gani kimewachelewesha hivyo?..mabasi mawili tayari yameshatupita. BIBIY: mwenzangu yote hayo ni kwa sababu ya huyu malkia wa urembo..ilinibidi kwanza nimlazimishe auoshe uso wake baada ya kujipaka vipodozi tele.. nilimwambia siwezi kutembea nae, alikuwa anaonekana kama kinyago haa! Rossie natamani ungemuona (anacheka). ROSSIE: Alaa!!! Ungemuacha aje hivyo hivyo ili namimi nipate kumuona.. ALMA: Ok ..tosha jamani yameisha hayo ...angalieni basi letu hilo linakuja. (Sauti ya basi) Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 4 MUSIC SCENE TWO (Muziki taratibu ndani ya salon) BEAUTICIAN: Kwa hiyo wasichana kama nilivyokwisha kuwaeleza ni lazima mtambue kuwa ni jambo la muhimu kulinda uzuri wa asili..sio vizuri kama vile wasichana wengine wanavyo anza kutumia krimu za kujichubua au wengine wanarukia tu madawa ya kutengeneza nywele..ni vyema msichana kujiringia uzuri wake wa asili..krimu za kujichubua ngozi madhara yake ni muda mrefu yanaweza kuathiri ngozi yako milele! ROSSIE: Aunty mimi huwa natamani kujua wasichana wengine huwa wanatumia nini kinacho wafanya ngozi zao kupendeza namna ile? BEAUTICIAN: sikiliza nikwambie, kuwa mdadidisi sana kupita kisai ndio mara nyingine kunawaponza wasichana hadi wakaingia mtegoni.. ingekuwa bora kama mara kwa mara mngewauliza mama zenu..muulize mama yako je alikuwa anafanya nini wakati yeye alipokuwa msichana, alikuwa anatumia nini .. mtashangaa huenda siri yake ya urembo ni vitu ambavyo vinapatika hapo hapo nyumbani labda hata ni bidhaa asilia zinazotumika jikoni kila siku. ALMA: Mimi ningetaka kujua kuhusu mbinu za kuziweka nywele zangu vizuri na staili ganiya nywele inapendeza zaidi? BEAUTICIAN: Alma..usiangalie kichwa cha mtu mwingine halafu ufikirie kuwa labda staili yake itakupendeza pia wewe..staili ya nywele inategemea sura yako..kwa mfano mwangalie huyu rafiki yenu Bibiy staili yake ya kusokota nywele inampendeza sana kwa sababu imekubaliana na sura yake.. zitunze nywele zako,ziweke safi wakati wote na epuka watalaamu wa nywele wasio na ujuzi!! Bibiy nakupongeza Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 5 nywele zako zinapendeza sana. BIBIY: Asante sana Aunty.. natumai rafiki yangu Alma amejifunza mengi kwa sababu anataka kuwa model hiyo ndio ndoto yake..Aunty kuhusu ile shughuli yetu ya shule sijui kama bado unakumbuka kuwa tunahitaji msaada wako katika kuandaa maonyesho ya urembo na mavazi?. BEAUTICIAN: Ndio nakumbuka Bibiy ...hata hivi nimechagua nguo kadhaa ambazo ningetaka mzijaribu ili tuamue kila mmoja wenu atavaa zipi wakati wa maonyesho, vilevile leo tutajifunza namna ya kutembea kwenye jukwaa. ALMA: Yuhuu!..nafurahi sana ..napenda maonyesho ya mavazi naona kweli ndoto yangu imeanza kufanikiwa! . Hee nasema siku moja mimi nitakuwa model tu!! BEAUTICIAN: Ok.. basi tuanze na wewe hebu njoo hapa nikubadili kidogo mtindo wa nywele zako halafu ukajaribu nguo hii hapa..nina hakika maonyesho yenu yatafanikiwa na yatakuwa gumzo la mji huu..nataka tufanye maonyesho ambayo hayajawahi kufanyika katika mji huu. ROSSIE: Yeah!! Hata mimi naamini tutafanikiwa ...mwalimu wetu pia ametusaidia sana katika matayarisho yaani tunaisubiri siku hiyo kwa hamu kubwa BIBIY: Sherehe hizi ni muhimu sana kwetu kwa kuwa tunasherehekea mafaniko yetu ya darasani na nje ya darasa. BEAUTICIAN: Anhaa! vizuri sana ... sasa hebu niwakumbushe kitu kimoja kuhusu urembo..ni muhimu sana kutunza urembo wenu hata kama wewe sio model, ninafahamu kuwa wasichana wengi wangependa kuwa mamodel lakini mjue kuwa sio wote watakao timiza ndoto hiyo.. ushauri wangu ninawaambia.. fanyeni bidii kwenye masomo yenu ili mtimize malengo yenu lazima mjiamini..Ok hebu sasa tuanze mafunzo yetu ya mwendo wa kimodel.. anza Alma.. Eenhee!!! vizuri sana hivyo Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 6 hivyo lakini pole pole kidogo.. Bibiy hebu kavae nguo hii hapa ili na wewe tukuone. ( Muziki taratibu) ROSSIE: Ooh! Nguo hiyo ni nzuri sana ..unapatia kabisa Bibiy ..Loo! umependeza sana. BEAUTICIAN: Biby utembee hivyo hivyo kwa maringo siku hiyo ya maonyesho.enhee mwingine atoke.. nakwambia.. siku hiyo kutakuwa na mambo jamani. Ambae hatafika basi atapitwa na mengi. BIBIY: Woow!! Alma rafiki yangu wewe ni model kweli sio mchezo.. unaonekana kama malkia wa urembo. ALMA: Ooh!...hata siamini Biby...angalia wala sijajipaka chochote usoni lakini napendeza. BEAUTICIAN: Enhee unaona sasa ninacho maanisha pale ninapo sisitiza urembo wa asili..haina haja ya kujichubua..Ok.. Rossie zamu ni yako sasa lazima turudie zoezi hili mara kadhaa ili msije mkafanya makosa siku ya maonyesho. (Muziki taratibu) BIBIY: Tumeshukuru sana Aunty kwa yote uliyotufanyia, lakini sasa inatubidi tuondoke kwa sababu tunataka kupitia kwenye internet cafe ili tukasome ujumbe na pia tunataka kutafiti mambo kadhaa. BEAUTICIAN: Na mimi nimefurahi sana kwa kuwa nanyi siku ya leo..natumai mmefaidika na vidokezo vya urembo nilivyowapa..mkipata nafasi kesho mnaweza kuja tena kwa mafunzo zaidi nawatakia kila la kheri..kwaherini. ALMA:. Asante kwa mara nyingine tena. Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 7 BEAUTICIAN: Hamna wasiwasi mnakaribishwa sana! (Wasichana....bye!!) MUSIC SCENE THREE: (katika ukumbi wa shule,ma kelele, muziki). HEAD TEACHER: Tafadhali hebu kimya kidogo tuelewane jamani (Sauti zinafifia)..asanteni..Naam wageni mashuhuri, mabibi na mabwana pamoja na wanafunzi hamjambo nyote..kwa niaba ya shule yetu ninawakaribisha kwenye sherehe hizi maalum ambapo wasichana wa shule hii wanasherehekea mafanikio makubwa waliyoyapata (Makofi) na moja kwa moja namkaribisha kiongozi wa kikudi cha wasichana cha Girl Power, si mwingine bali ni Bibiy..maarufu sana kwa jina la Bob Marley girl. (Makofi) KIBEGU: Wow!! ... Timo..kwa kweli msichana huyu ni sawa na nyota ..staili ya nywele zake inamfanya kila mtu akose la kusema. TIMO: Mimi nakwambia maneno yote niliyo jifunza hayatoshi kuueleza urembo wa Bibiy, sijui nimuite ”Cleopatra” au vipi ...sasa nakwambia Kibegu ...jitayarishe kurogwa na sauti yake nyororo..Loo! Bibiy kweli ni special. KIBEGU: Yeah!! Kila mtu katika mjii huu anamtaja yeye...,ni msichana mwerevu tena shupavu. TIMO: basi Kibegu nyamaza ...ndio huyo ameshapanda kwenye jukwaa. (Makofi) Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 8 BIBIY: Asanteni kwa makofi, shukurani wageni wote mliofika..(Makofi, mbinja. Vigelegele, ngoma nk.) na kwa mujibu wa orodha yetu tutaanza kwa maonyesho ya mavazi na urembo..karibuni sana. (Makofi) MUSIC HEAD TEACHER: Basi huo ndio tunauita ubunifu..kwa kweli wasichana leo hii wametuonyesha mambo mengi mpaka hata mimi mwenyewe mwalimu mkuu nimejawa na furaha kuona kuwa wasichana wamepata mafanikio makubwa.. wameonyesha uwezo mkubwa katika masomo na michezo pia na hakika uwezo wao hauna tafauti na ule wa wavulana, wanaweza kutekeleza yote sawa na wavulana.. basi tuendelea mbele na tafrija zetu.. sasa namkaribisha Rossie, nae ametuandalia shairi. (Makofi) ROSSIE: Asanteni shairi langu ni kuhusu ujasiri na walengwa ni wasichana wote popote pale walipo. Ujasiri unaleta nguvu Ujasiri unaondoa woga Ujasiri unaleta matumaini na ushindi Ujasiri unakupa moyo wa kuendelea kupambana Kama vile uko juu ya mgongo wa farasi Ujasiri unakufikisha kwenye malengo yako Kwa hekima bila utata. Asanteni!! (Makofi) MUSIC KIBEGU: Bibiy naomba tucheze pamoja. Noa bongo Jenga maisha yako : Learning by Ear Kuwajenga wa wasichana Nr.10 9 BIBIY: hamna shida leo ni siku yetu..loo! Kibegu asanteni sana kwa kutusaidia ..ukumbi unapendeza kweli. KIBEGU: Unajua Bibiy wakati sasa umewadia ambapo wavulana lazima tukubali kuwa wasichana pia wana uwezo kama sisi..nadhani inabidi tuchukulie kushindwa kwetu kuwa ni changamoto kutoka kwa wasichana ... Bibiy jitihada zako zimeleta mabadiliko makubwa katika mji wetu natumai wasichana wote wataiga moyo wa kikundi chenu cha Girl Power hongera sana Bibiy. BIBIY: Asante sana Kibegu, maneno yako ya busara yatatuongoza kwa muda mrefu. Hakika tutaendeleza juhudi zetu kila siku, tutamulika maswala mbali mbali yanayotukabili sisi wasichana na tutajitahidi kuyatafutia ufumbuzi..natumai Girl Power itakuwa kielelezo. MUSIC Outro: Naam hatimae wavulana wamekubali kuwa wasichana wana uwezo kama wao. Wasichana nao wamekata kauli kuendeleza jitihada za kuyatafutia ufumbuzi maswala mbali mbali yanayowakabili. Na mpaka hapo ndio nasi tumekamilisha sehemu ya kumi ya mchezo wa kuigiza katika makala ya Jifunze Kwa kusikiliza.Usikilize tena mchezo huu pia mwambie rafiki yako ausikilize kupitia kwenye tovuti yetu www.dwworld.de/lbe Shukurani kwa kuwa nasi...Kwaheri. END

No comments:

Post a Comment

Adbox

@EmmyGraphicsPrinting